Djokovic azama nusu fainali kilaini Australian Open 2019
Bingwa mara 6 wa Australian Open Novak Djokovic amefuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo baada ya mshindani wake katika mchezo wa robo fainali leo Mjapan Kei Nishikori kushindwa kuendelea na mchezo kufuatia kupata maumivu ya paja.
Wakati Kei Nishirikori anapata maumivu hayo Novak alikuwa anaongoza kwa seti 6-1, 4-1.
Kila muda ambao Mserbia huyo amefika katika nusu fainali ya michuano hiyo,huwa anachukua ubingwa
Novak ambaye ni namba 1 kwa ubora duniani kwa upande wa wacheza tenesi wanaume, atacheza na Mfaransa Lucas Pouille katika hatua hiyo ya nusu fainali.
Nusu fainali nyingine itakuwa ni kati ya Mhispania Rafa Nadal na Mgiriki Stefanos Tsitsipas mwenye umri wa miaka 20.