De Gea aweka viatu vyake kwenye Frame
Kipa wa Man United David de Gea ameviweka Frame viatu alivyovaa katika mechi dhidi ya Tottenham iliyochezwa Januari 13 katika uwanja wa Wembley
Katika mechi hiyo ambayo United walishinda 1-0, De Gea aliokoa michomo 11 ambayo ni mingi katika mechi moja ya ligi kuu nchini England msimu huu kuliko aliyofanya kipa mwingine yoyote.
De Gea aliweka picha hiyo ya viatu vikiwa kwa Frame katika mtandao wa Twitter huku akimsifia mtangazaji wa mechi wa Sky Sports Martin Tyler kwa kumpa wazo hilo.