Kutana na Mtanzania anayekipiga Portsmouth
Beki wa kulia Muingereza mwenye asili ya Tanzania Haji Mnoga mwenye umri wa miaka 16 jana kwa mara ya nne amepata nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza cha Portsmouth ambapo walishuka dimbani kucheza na Peterbrough .
Katika mechi hiyo beki huyo alicheza dakika 90, timu yake ikishinda goli 1-0.
Mwezi Oktoba mwaka jana @hajimnogax aliweka rekodi ya mchezaji mdogo namba mbili kuichezea Portsmouth akiwa na umri wa miaka 16 miezi mitano na siku 23.