Serena Williams atupwa nje Australian Open 2019
Bingwa mara 7 wa Australian Open Serena Williams ametolewa katika hatua ya robo fainali ya michuano hiyo baada ya kufungwa kwa seti 4-6,6-4,5-7 na Karolina Pliskova kutoka Czech.
Serena katika seti hiyo ya mwisho ya kuamua nani aende nusu fainali alikuwa anaongoza 5-1, Pliskova akafanya comeback na kushinda 7-5.
Pliskova katika hatua ya nusu fainali atakutana na bingwa wa US Open mwaka jana Mjapan Naomi Osaka kesho alhamisi.