GARY LINEKER AMBADILIKIA RONALDO KUHUSU KUPOST PICHA AKIWA KATIKA NDEGE YAKE BINAFSI
Mchambuzi na mtangazaji Gary Lineker amemgeukia nakumkosoa nyota wa klabu ya Juventus ya nchini Italia Cristiano Ronaldo kufuatia kupost picha akiwa kwenyendege yake binafsi, Lineker hajapenda kwa Ronaldo kupost picha hiyo akiwa kwenye ndege yake binafsi kwawakati huu.
Lineker ameamua kumkosoa nyota huyo kutokana nauamuzi wake wa kupost picha akitabasamu akiwakwenye ndege yake binafsi, wakati huu ambao dunia yasoka ina majonzi kwa kupotea kwa ndege aliyokuwaamepanda nyota wa Cardiff City Emiliano Sala usiku waJanuari 21 “Sio siku ya kupost hii tweet, kiukweli sio”
Ndege hiyo aliyokuwa kapanda Emiliano Sala na rubaniimepotea wakiwa wanatoka Nantes kurudi Cardiff, baadaya mchezaji huyo kusaini mkataba wa kuichezea Cardiff City Jumamosi akitokea Nantes, alipewa ruhusa maalumya kurudi Nantes kuaga wachezaji na uongozi wa timu hiyo.
Baada ya Emiliano kutekeleza dhamira yake hiyo wakatianarudi akiwa kwenye ndege binafsi na rubani, ndegehiyo mamlaka ya anga nchini Ufaransa wamethibitishakuwa ilipotea, inasadikika ndege hiyo imepata ajali nakuanguka bahari ila taarifa rasmi bado hajizathibitikalakini jopo la uopoaji limeondoa matumaini yakupatikana kwa watu hao wakiwa hai.