Morata kurudi kwao Hispania
Baada ya kudumu na timu ya Chelsea kwa miezi 18 nyota wa kihispani Alvaro Morata ameripotiwa kuwambioni kurudi kwao Hispania baada ya kocha waChelsea Maurizio Sarri kuonesha kuwa hayupo kwenyemipango yake nyota huya ambaye kwa hivi karibuniamekuwa akiisaka namba.
Morata (26) anarejea Hispania katika timu ya AtleticoMadrid kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu Ila mkataba huo wa mkopo una kipengele cha kumnunuajumla mwisho wa msimu kwa ada ya pauni milioni 48.5 taarifa hizo zinaashiria kuwa Morata anarudi nyumbanikatika jiji la Madrid mji ambao ndio amezaliwa.
Tukukumbushe tu Morata ambaye ameonekana hananafasi baada ya ujio wa Maurizio Sarri katika timu hiyo, alijiunga na Chelsea 2017 majira ya usajili ya jotoakitokea Real Madrid kwa ada ya uhamisho ya rekodi yapauni milioni 60 na msimu wa kwanza aliifungia timuhiyo mabao 15 katika michezo 23.