Glen Johnson atandika daruga
Beki wa zamani wa Liverpool na timu ya Taifa ya England Glen Johnson ametangaza rasmi kustaafu kucheza soka akiwa na umri wa miaka 34.
Katika miaka ya 16 ya kucheza soka, Johnson amecheza vilabu vya West Ham, Chelsea, Portsmouth, Liverpool na Stoke City.
Pia alicheza timu ya Taifa ya England mechi 54 kati ya mwaka 2003 na 2014, akiiwakilisha kwenye michuano ya kombe la Dunia mara mbili na michuano ya Euro.
Johnson ambaye aliachwa na Stoke City baada ya kushuka daraja kutoka Premier League msimu uliopita, ametangaza kustaafu leo jumatatu asubuhi kupitia redio ya Talksport ya huko England.
Johnson amewahi kushinda kombe la Premier League, FA Cup na Kombe la ligi.