Kilichomkuta Serena chamkuta Federer
Baada ya kumuona Naomi Osaka akimfunga Idol wake Serena Williams katika fainali ya US Open mwaka jana, katika Australian Open tumeshuhudia stori hiyo tena.
Roger Federer ,37, ametolewa katika raundi ya nne ya michuano hiyo na Mgriki Stefanos Tsitsipas mwenye umri wa miaka 20 akiwa katika nafasi ya 14 katika viwango vya ubora wa tenesi duniani kwa wanaume.
Mswiss huyo ambaye anashika nafasi ya 3 katika viwango vya ubora wa tenesi duniani amefungwa kwa seti
7-6,6-7,5-7,6-7.
Federer bingwa mara 6 wa Australian Open, sasa ameshindwa kufika robo fainali ya michuano hiyo kwa mara ya pili katika miaka 16.
.
“ Ni mtu mwenye furaha zaidi kwa sasa duniani. Siweze kuelezea. “amesema Tsitsipas
.
“ Nimemfunga Idol wangu. Idol wangu leo alikuwa ni mpinzani wangu. “
.
Baada ya kutolewa kwenye michuano hiyo Roger Federer amesema kuwa mwaka huu atacheza French Open baada ya kutoshiriki michuano hiyo kwa miaka miwili mtawalia.