JOSE MOURINHO KAWATAJA KLOPP NA GUARDIOLA KUWA NDIO MAKOCHA WENYE RAHA ZAIDI EPL WAKATI AKIWA KOCHA
Kocha wa zamani wa Manchester United Jose Mourinho leo alipata nafasi ya kuwa mchambuzi katika kituo cha BeinSports wakati wa mchezo wa ligi Kuu nchini London kati ya Arsenal waliokuwa nyumbani dhidi ya Chelsea, hatimae dakika 90 kumalizika kwa Arsenal kupata ushindi wa 2-0.
Mourinho akiwa anachambua mchezo huo ambao ukihusisha timu yake ya zamani ya Chelsea ameongea mambo mengi ikiwemo kawataja makocha wenzake Pep Guardiola wa Manchester City na kocha Jurgen Klopp wa Liverpool kuwa hao walikuwa na maisha mazuri zaidi EPL zaidi yake.
Jose Mourinho alielezea kuwa makocha hao walikuwa wana raha kwa sababu walipata nafasi ya kuwachagua wachezaji wanaowataka na kujenga timu katika mfumo wanaoutaka tofauti na ilivyokuwa kwake wachezaji wengi aliwakuta na hakupewa nafsi ya kusajili kwa matakwa yake na kujenga kikosi chake.
“Kwangu ilikuwa ngumu kidogo kama meneja sikuwa nalenga tu kwenye mpira pia katika malengo yajayo lakini malengo pia yanaandaliwa kwa kanuni ukiangalia kama ishu ya Manchester City msimu wa kwanza Pep Guardiola hakuwa Bingwa na wengi walitegemea Ubingwa na makubwa kutoka Manchester City ila haikutokea” alisema Jose Mourinho

“Ilikuwa Manchester City inatoka katika kipindi cha Ubingwa cha Mancini na Manuel lakini pia baaadhi ya wachezaji walikuwa tayari Mabingwa mara mbili kama Aguero na Kompany lakini katika msimu wake wa kwanza kwenda wa pili Guardiola alifanya maamuzi mazuri ambayo yaliungwa mkono na uongozi” alisema Jose Mourinho