PATRICK AUSSEMS ‘UCHEBE’ KATAJA ALIPOZIDIWA NA AS VITA
Kiu ya watanzania na mashabiki wa Simba kuona mchezo wa pili wa hatua ya makundi wa michuano ya klabu Bingwa Afrika kati ya AS Vita dhidi ya Simba uliyopigwa katika mji wa Kinshasa, iliingia nyongo kufuatia kupoteza mchezo huo kwa mabao 5-0.
Baada ya mchezo kocha wa Simba Patrick Aussems na kocha wa AS Vita Ibenge kumbe walikuwa wamesoma pamoja, hivyo Aussems alikiri kuwa wanafahamiana vizuri na walichozidiwa ni uzoefu tu kufuatia wote kusoma chuo kimoja Ufaransa cha ukocha ila wachezaji wao ndio wametofautiana uzoefu.
“Sababu ya matokeo haya ni utofauti wa wachezaji wetu na wachezaji wa AS Vita hasa wanaposhindana mtu na mtu na Ukumbuke Vita msimu uliopita wamecheza fainali ya Kombe la shirikisho Afrika lakini Simba miaka 15 hajacheza makundi kwa hiyo tunahitaji muda kujijenga timu zaidi”.
Simba sasa kufuatia kipigo hicho cha 5-0 kilichozua gumzo mtandaoni, kinawashusha katika msimamo wa Kundi D kutokana nafasi ya pili hadi nafasi ya tatu kutokana na Kundi kuongozwa na Al Ahly ya Misri kwa alama nne, AS Vita wa pili alama tatu sawa na Simba ila wamewazidi mabao ya kushinda na kufungwa na JS Saoura ya Algeria ikiburuta mkia kwa kubaki na alama moja.