JACOB MASAWE AMEFICHUA SIRI KOCHA WAO ALIVYOWAJENGA KISAIKOLOJIA
Nahodha wa Stand United Jacob Masawe ambaye ndio aliifungia bao la ushindi Stand United dakika ya 88 dhidi ya Yanga, ameeleza kuwa kocha wao aliwatoa hofu mapema kabla ya mchezo na kuwaambia waingia wacheze mpira wasihofu kwani wachezaji wa kitanzania wanafanana tofauti yao ndogo sana.
Kauli au maelezo ya kocha wa Stand United kwa wachezaji wake yanaonekana kuwajenga kisaikolojia kiasi cha kuvunja rekodi ya Yanga kwa kuwa timu ya kwanza kuwafunga Yanga msimu huu katika Ligi Kuu, wakiifunga kwa bao 1-0, na kuwafanya waziache alama zote tatu mjini Shinyanga katika uwanja wa CCM Kambarage.
“Mwalimu alifanya kazi ya ziada kwa sababu ukizingatia tuna kikosi kidogo yeye alitujenga sisi kwamba mchezaji katika uchezaji wachezaji wa kitanzania tofauti ndogo sana, kwa hiyo baada ya mwalimu kutuambia tukaona mtu yoyote anayeweza kupata nafasi anaweza akaonesha kitu atakacho kifurahia , Yanga ni timu nzuri Yanga ni timu kubwa pamoja na kuwafunga lakini wamecheza vizuri”
“Kama kuna watu wana wabeza sio kweli Yanga ni timu nzuri Yanga ina wachezaji wazuri na ina mwalimu mzuri kwa hiyo sisi ushindi huu kwanza tunamshukuru Mungu kwakweli” alisema Jacob Masawe baada ya mechi
Yanga wanabaki kieleni licha ya kipigo cha bao 1-0 lililofungwa dakika za lalama salama ila Stand United wamefikisha jumla ya alama 25 Yanga wakiwa na alama zao 53 walizovuna katika michezo 19 ya Ligi Kuu, Stand United ndio timu iliyovunja rekodi ya Yanga kucheza kwa mechi 19 pasipo kupoteza mchezo hata mmoja, Stand inaenda kukaa nafasi ya 12 katika msimamo wa Ligi Kuu.