CHILUNDA ATOLEWA KWA MKOPO HISPANIA
Mchezaji wa kitanzania aliyejiunga na klabu ya CD Tenerife akitokea Azam FC Shaban Iddi Chilunda ameripotiwa kujiunga na klabu ya CD Izzara ya nchini Hispania pia kwa mkopo wa muda mfupi, Chiliunda ambaye ni mchezaji mahiri atadumu katika klabu hiyo hadi mwisho wa msimu.
Chilunda alijunga na CD Tenerife kwa kandarasi ya miaka miwili akitokea Azam FC aliyokuwa anaichezea tokeo team B, hivyo CD Tenerife wanaoshiriki Ligi daraja la kwanza (Segunda Division) wamefikia maamuzi ya kumtoa kwa mkopo wa muda mfupi nyota huyo.
Tukukumbushe tu Shaban Iddi Chilinda alijiunga na CD Tenerife Agosti 2018 akitokea Azam FC kwa nusu msimu uliosalia atakuwa akicheza CD Izzara hadi uishe, timu ambayo inashiriki Segunda Division B, hata hivyo pamoja na kutolewa kwa mkopo Chilunda anatajwa kuja kuifanyia makubwa Tenerife kwa siku za usoni.