AARON RAMSEY AMESAINI MKATABA WA AWALI NA JUVENTUS
Wakati kukukiwa na taarifa za kudai kuwa kocha mkuu wa Arsenal Unai Emery yupo radhi Mesut Ozil aondoke Arsenal, nchini Italia zimeripotiwa taarifa za Mabingwa wa Super Coppa klabu ya Juventus kufikia makubaliano na kiungo wa Arsenal Aaron Ramsey.
Taarifa iliyoelezwa kuripotiwa na Sky Sports Italia inaeleza kuwa Aaron Ramsey tayari amesaini mkataba wa awali na Juventus utakaomuwezesha kulipwa mshahara wa pauni 300,000 ila Juventus wenyewe wamepanga kutangaza taarifa hizo mwezi Februari.
Kiungo huyo inaelezwa kuwa tayari ameshafanya vipimo vya afya weekend hii na amesaini (Pre Cotranct) ambayo itatangazwa rasmi na Juventus mwezi Februari ila mchezaji huyo atajiunga na Juventus mwisho wa msimu, Ramsey alijiunga na Arsenal 2008 akitokea Cardiff City na ameichezea Arsenal jumla ya michezo 253 na kuifungia mabao 53.