PATRICK AUSSEMS AWEKA WAZI HAKUNA KUJIHAMI CONGO
Timu ya Simba leo, Januari 19 2019 itakuwa uwanjani kucheza mchezo wa pili wa hatua ya makundi ya klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo ambao tayari walishapoteza mchezo wao wa kwanza kwa kufungwa 2-0 na Al Ahly nchini Misri.
AS Vita wanaingia katika mchezo huo wakiwa hawana alama hata moja ila wanaonekana kuwa wanaweza kupata matokeo chanya dhidi ya Simba kwa kuwa katika uwanja wao wa nyumbani mjini Kinshasa, kocha mkuu wa Simba SC Patrick Aussems ameweka wazi mfumo wake atakaotumia katika mchezo huo.
Mapema katika mkutano na waandishi wa habari Aussems aliyekuwa ameambatana na nahodha wake msaidizi Haruna Niyonzima alieleza kuwa lengo lake ni kuondoka Kinshasa akiwa na alama tatu na hawezi kucheza mchezo wa kujihami na kujilinda kama ilivyokuwa inatazamiwa na wengi michezo ya ugenini kuchezwa kwa mfumo huo.
“Itakuwa mechi ngumu lakini hatujaja hapa kuzuia, tumekuja hapa kujaribu kutengeneza nafasi kama ilivyo kwa michezo yetu mingine na kujaribu kufunga.”alisema kocha wa Simba SC Patrick Aussems