Chamberlain kurejea kabla msimu kuisha
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp amesema kuwa winga Alex Oxlade Chamberlain atarejea katika kikosi cha ndani ya msimu huu.
Mchezaji huyo amekuwa nje ya uwanja tangu April 2018 alipoumia goti lake katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali klabu bingwa Ulaya dhidi ya AS Roma.
Hapo awali ilielezwa kuwa mchezaji huyo anahitaji miezi 12 ili kupona,lakini tayari Muingereza huyo ameonekana kuanza kufanya mazoezi tayari kujiweka sawa kurejea uwanjani.