Usiku wa Red Bull
Katika mbio za Mexico Grand Prix timu ya Red Bull imefanya vyema kwenye mbio za michuano na kufanikiwa kushika nafasi mbili za juu. Daniel Riciardo ndie aliyechukua Pole position mbele ya dereva mwenzake wa Red Bull Max Vertapen baada ya kumpita kwa sekunde 0.062 baada ya Max kuwa ameongoza na kufanya vizuri mizunguko yote kabla ya kuja achwa katika mzunguko wa mwisho kwa muda huo kidogo kabisa ambao ulimpa hasira.
Hii ni mara ya kwanza kwa Red Bull kushika nafasi za mbili za juu tokea mwaka 2013 kwenye US Grand Prix na ni pole position yao ya 60.
Zilikuwa mbio zilizojaa vionjo, hisia na ushindani hasa kutoka katika timu ya Red Bull kufanya vizuri kwenye mbio hizi za awali dhidi ya mahasimu wawili Mercedes na Ferrari.
Nafasi ya tatu imechukuliwa na Lewis Hamilton akiwa mbele ya hasimu wake Sebastian Vettel huku nafasi ya tano ikichukuliwa na Bottas na ya sita ikienda kwa Kimmi Raikkonen. .
Ili kuendelea weka hai matumaini ya ubingwa Vettel anahitaji shinda mbio hizosikubya kesho na Lewis Hamilton amalize katika nafasi ya 8 kushuka. Vettel hajawahi shinda mbio akianzia nje ya nafasi 3 za juu.
Kwa Hamilton anahitaji shika nafasi 7 za juu ili kujihakikishia ushindi.
Mbio zitafanyika hapo kesho siku ya Jumapili huku dereva Lewis Hamilton akihitaji points 5 tu ili kujihakikishia ubingwa kwa mara ya 5.