Man United ushindi nje ndani
Kiungo wa Man United Fred pamoja na mkewe Monique Salum wamefanikiwa kupata mtoto wa kiume ambaye wamemuita jina la Benjamin.
Mtoto huyo ambaye mtoto wao wa kwanza amezaliwa jumatano hii Januari 16.
Huu ni mfululizo kwa wachezaji wa Man United kupata watoto kwa kipindi hiki.
Romelu Lukaku na mpenzi wake Sarah walipata mtoto wa kiume kabla ya Christmas, Paul Pogba na mpenzi wake nae Maria Salaues nao wamepata mtoto wao wa kwanza katika mwaka huu mpya na Nemanja Matic pamoja mke wake Aleksandra hivi karibuni wamepata mtoto wao watatu.
Neema ya kupata watoto haijaishia hapo Old Trafford, Victor Lindelof, Chris Smalling na Matteo Darmian wapenzi wao wana ujauzito , hivyo wanatarajia kupata watoto.