Bikosports wadhamini Tuzo za Ligi Kuu Tanzania Bara
Kampuni ya Bikosports leo imetangaza kuwa wadhamini wa tuzo za mchezaji bora na kocha bora wa mwezi katika ligi kuu Tanzania bara.
Mshindi wa tuzo ya mchezaji bora ambayo imekuwa ikitolewa na bodi ya ligi kuu sasa itakuwa ikitolewa na kampuni hiyo ya ubashiri wa matokeo ya michezo.
Bikosports kupitia msemaji wake Geoffrey Lea leo wameahidi kuwa watakuwa wakitoa Kitita cha Tsh milioni moja kwa mchezaji bora na Tsh Milioni Moja kocha bora wa mwezi sambamba na tuzo ambayo itakua ni kumbukumbu kwa mshindi.
Zoezi hili linaanzia kwa mchezaji bora wa mwezi Disemba Heritier Makambo na kocha bora mwezi huo Mwinyi Zahera, wote kutoka katika klabu ya Yanga na kuendelea mpaka mwisho wa msimu huu.