MWINYI ZAHERA KATOA USHAURI KWA SIMBA KUELEKEA MCHEZO DHIDI YA AS VITA
Kocha wa Yanga raia wa Congo na Ufaransa Mwinyi Zahera akiwa anaelekea Shinyanga kucheza mchezo wake wa Ligi Kuu dhidi ya , alifanya mahojiano maalum na Azam TV na kuulizwa ushauri wake kuhusiana na Simba SC waliosafiri kuelekea Congo kucheza dhidi ya AS Vita Jumamosi ya Januari 19 2019.
.
“Simba anapaswa kucheza kwamba tunacheza kwa lengo la kucheza na kushinda, kama unaenda kusema tunaenda kusema tucheze tujilinde hiyo itakuwa ngumu sana kwa Simba ila kama watasema wacheze wajilinde wapate sare hiyo mechi itakuwa ngumu ila kama watacheza kwa lengo la kucheza kabisa na kushinda sio kujiami huo mchezo utakuwa rahisi kwake” alisema Mwinyi Zahera.
Simba SC imefanikiwa kushiriki michuano ya Klabu Bingwa Afrika hatua ya Makundi mwaka huu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15, wamepangwa Kundi D lenye timu za Al Ahly ambao ni Mabingwa wa kihistoria wa michuano hiyo, AS Vita na timu changa katika michuano hiyo JS Saouro ya Algeria iliyoanzishwa mwaka 2008.