Bocco awakosa wacongo
ODaktari wa Simba SC Yassin Gembe amesema John Bocco ataukosa mchezo dhidi ya AS Vita jumamosi hii kutokana na kuwa na maumivu ya nyama za paja.
Daktari huyo ameeleza hayo kupitia mahojiano aliyofanyiwa na Azam TV.
Nahodha huyo alipata maumivu hayo katika mchezo wa jumamosi iliyopita dhidi ya JS Saoura jijini Dar es salaam.
Simba wameondoka leo jijini Dar es kueleka nchini Congo kwa ajili ya mchezo wao huo wa pili katika hatua ya makundi.