Dembele afuata pesa za wachina
Guangzhou R&F ya ligi kuu nchini China imemsajili kiungo Mousa Dembele kutoka Tottenham Hotspur kwa kandarasi ya miaka mitatu.
Dembele ambaye alikuwa amebakisha mkataba wa miezi 6 katika klabu ya Tottenham ametua katika timu hiyo kwa ada ya pauni milioni 11
Mbelgiji huyo,31, ameichesa Tottenham mechi 249 katika michuano hiyo tangu ajiunga nayo mwaka 2012 akitokea Fulham.