Abramovich hafikiri kuiuza Chelsea
Tajiri Roman Abramovich hana mpango wa kuiuza klabu ya Chelsea ya nchini England tofauti na ripoti nyingi zinavyoeleza. Tetesi zimekuwa zikienea kuwa tajiri namba moja wa Jamuhuri ya Czech, Petr Kellner amekuwa na nia ya kuinunua klabu hiyo lakini kituo cha Sky kimeripoti kuwa hakuna maongezi yaliyofanyika au yanayoendelea baina ya mmiliki wa Chelsea na mwekezaji mwingine yeyote.
Tajiri huyu Mrusi amekumbwa na sekeseke la visa yake ya Uingereza iliyomsababisha kukosa fainali ya kombe la FA kati ya Chelsea dhidi ya Manchester United na kusababisha minongono ya sintofahamu juu ya hatma yake na klabu hiyo ya jijini London.
Aliinunua Chelsea mwaka 2003 kwa Pauni 140 millioni na tokea hapo klabu hii imefanikiwa chukua jumla ya mataji 17, Klabu bingwa ulaya 1, Ubingwa wa ligi ya Europa 1, Ubingwa wa ligi kuu 5, Kombe la FA 5, Kombe la ligi 3 na Ngao ya Hisani mara 2.