EDO KUMWEMBE KAMUANGALIA GYAN KWA JICHO LA PILI
Edo Kumwembe ni moja kati ya wachambuzi mahiri Tanzania na amekuwa akifanya chambuzi na tathmini mbalimbali kuhusiana na mchezo wa soka, hiyo inatokana na uelewa wake katika mchezo wa soka na kipawa chake cha kuchuja na kuchambua mambo.
Imewahi kusikika kwa baadhi ya wachezaji Afrika wakipishana na walimu kutokana na kupangwa nafasi tofauti, ila Edo Kumwembe ameamua kusifia nidhamu ya mchezaji raia wa Ghana anayecheza Simba SC Nikolaos Gyan ambaye aliletwa Simba kama mshambuliaji na waalimu kuamua kumtumia kama beki wa pembeni na ameendelea kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu pasipo kupishana na waalimu.

Baadhi ya wachezaji Ulaya kama Gareth Bale wa Real Madrid aliwahi kuwa beki lakini waalimu walipomuangalia uwezo wake wa kucheza na kasi yake uwanjani, wakaona anastahili kucheza nafasi za mbele, Edo Kumwembe ameshinda kuvumilia ameamua kuandika haya kupitia ukurasa wake wa Instagram kuelezea nidhamu ya hali ya juu ya Gyan
“Huyu mchezaji anaitwa Nicolas Gyan…kwangu ndiye Professional halisi kwa kipindi cha miaka miwili iliyopita alikuja nchini akitajwa kuwa striker hatari sana…hakuwika akarudishwa kuwa beki wa kulia, hakuhama timu wala hakuhama Nchi, akaipokea nafasi akaebdelea kujituma ndivyo inavyobidi kambi popote”
“Uwepo tu katika timu na kupambana kwa machozi, jasho na damu. Kuna wa kwetu ambao nawafahamu. Kwanza wasingekubali pili kila siku wangekuwa wanalalamika katika magazeti..huyu jamaa anakimbiza tu kimya kimya ili mradi mshahara wake uingie na ili mradi umuhimu wake katika timu uendelee Ndo wachezaji halisi wa West Africa walivyo Typical professional. Mwanadamu anaishi mara moja tu…kambi popote…Typical Professional footballer I SALUTE YOU BRO “