Mnyama kuwafuata wacongo kesho
Baada ya kushinda mchezo wao wa kwanza katika hatua ya makundi wikiendi iliyopita, klabu ya Simba inataraji kuondoka Tanzania hapo kesho Alhamisi Januari 17 na kuelekea jijini Kinshasa nchini Congo kwa ajili ya mchezo wa pili hatua ya makundi ambao watacheza dhidi ya AS Vita
Mchezo huo unataraji kucheza siku ya jumamosi Januari 19 saa 11 jioni kwa saa za Congo ambapo kwa Tanzania itakuwa ni saa moja usiku
Simba SC wanataraji kukutana na upinzani mkali kutoka kwa AS Vita kufuatia timu hiyo kupoteza mchezo wao wa kwanza wa kundi ambao walicheza dhidi ya Al Ahly nchini Misri.