CAF yaipa adhabu Esperance
Shirikisho la mchezo wa mpira wa miguu barani Afrika CAF limetangaza maamuzi mazito baada ya kikao chao cha kamati ya maadili kukutana na kujadili nidhamu ya mashabiki wa timu ya Esperance ya Tunisia waliyoioneshwa wakati wa mchezo wa fainali ya klabu Bingwa Afrika Msimu uliopita.
CAF kwa maridhiano ya pamoja imeamua kuifungia klabu ya Esperancepo mechi mbili za klabu Bingwa Afrika kucheza pasipo uwepo wa mashabiki, mechi hizo zitakuwa za makundi za michuano ya klabu Bingwa Afrika msimu huu, hiyo ikiwa sehemu ya kutoa onyo kwa mashabiki hao.
Mashabiki wa Esperance walileta vitendo visivyo vya kiungwana michezoni wakati wa mchezo wa fainali ya klabu Bingwa Afrika mwaka 2018, hivyo CAF wamefikia maamuzi hayo kama sehemu ya kuwarekebisha.
Esperence ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo baada ya kuifunga Al Ahly mwaka jana katika mchezo wa fainali, msimu huu wamepangwa Kundi B lenye timu za Horoya, FC Platnum na Orlando Pirates.