Cech kutundika daruga
Baada ya miaka 20 ya kucheza soka kipa wa klabu ya Arsenal Peter Cech ametangaza kuwa atastaafu kucheza mchezo huo mwisho wa msimu huu.
Kipa huyo,36, kutoka nchi ya Jamhuri ya Czech ametangaza hivyo leo kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter.
“ Huu ni msimu wangu wa 20 nikiwa mchezaji Professional na imekuwa miaka 20 tangu nisaini mkataba wangu wa kwanza wa Professional, sasa ninahisi kama ni muda sahihi kutangaza kwamba nitastaafu mwishoni mwa msimu huu “
“ Nimecheza miaka 15 katika Premier League na kushinda kila kombe lililowezekana, ninajihisi nimefanikiwa kila kitu nilichopanga kufanikisha “ ameandika Cech.
Akiwa na timu za Chelsea na Arsenal Cech ameshinda jumla ya makombe 18 ambapo makombe ya Premier League ni manne na klabu bingwa Ulaya ni moja.