Mchezaji wa Azam aitwa timu ya taifa Ghana
Mara nyingi imekuwa ni nadra sana kwa wachezaji wa Afrika Magharibi wanaocheza soka katika nchi za Afrika Mashariki kupata nafasi ya kuitwa katika vikosi vya timu zao za taifa, hii inatokana na kuwa na wachezaji wengi wa Afrika Magharibi kucheza soka barani Ulaya na makocha kuwekeza nguvu zaidi huko.
Makocha wa timu za taifa za Afrika Magharibi wa ngazi zote wamekuwa na utamaduni wa kupenda kuwafuatilia wachezaji wa mataifa yao wanaocheza Ulaya zaidi au Afrika katika nchi zenye Ligi Kubwa, hii imekuwa tofauti kwa winga wa Azam FC Enock Atta uwezo wake wa kipekee umempa nafasi.
Enock Atta leo Azam FC wametangaza kupokea taarifa za kuitwa kwa mchezaji huyo katika kikosi cha timu ya taifa ya Ghana kwa wachezaji wenye umri chini ya miaka 20, kikosi ambacho kitacheza fainali za Mataifa ya Afrika AFCON U-20 zitakazofanyika nchini Niger ambazo zitaanza Februari 2 hadi 17 2019.