LIONEL MESSI JINA LAKE LINAZIDI KUJAA KATIKA VITABU VYA HISTORIA VYA FC BARCELONA
Mshambuliaji na nahodha wa timu ya taifa ya Argentina na klabu ya FC Barcelona ya nchini Hispania Lionel Messi pamoja na kujizolea umaarufu mkubwa duniani kote kutokana na umahiri wake katika soka na kuweka rekodi mbalimbali, jina lake linazidi kuwekwa katika vitabu vya kumbukumbu kila kukicha.
Lionel Messi jana akiiongoza FC Barcelona kucheza mchezo wao wa 19 wa Ligi Kuu ya nchini Hispania dhidi ya Eibar, amefanikiwa kuifungia bao timu hiyo katika ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Eibar, magoli ya Barcelona yalifungwa na Luis Suarez aliyefunga mabao mawili dakika ya 19 na 59 na Lionel Messi dakika ya 53 bao ambalo limemfanya kuendelea kuweka Legacy Nou Camp.
Baada ya kufunga bao hilo Lionel Messia anaweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza katika historia ya Ligi Kuu ya Hispania kufunga jumla mabao 400 katika Ligi hiyo kukiwa hakuna mchezaji yoyote aliyewahi kufikia rekodi hiyo kabla ya Lionel Messi kuiweka dhidi ya Eibar, goli lake la kwanza Lionel Messi katika Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama LaLiga alifunga miaka 14 iliyopita.
Hata hivyo ushindi huo pia unaifanya Barcelona iendelee kuongoza Ligi hiyo kwa kuwa na alama 43 tofauti ya alama 5 na Atletico Madrid anayefuatia, tukukumbushe tu Lionel Messi alijiunga na kituo cha kukuzia vipaji cha FC Barcelona (La Masia) mwaka 2001 akitokea Newell’s Boys ya kwao Argentina kabla ya mwaka 2004 kufuzu na kufikia vigezo vya kupandishwa kucheza timu ya wakubwa.