Kerr ashinda tuzo ya kocha bora Kenya
Aliyekuwa kocha wa klabu ya Simba ya Tanzania bara Dylan Kerr ametwaa tunzo ya kocha bora wa mwaka katika ligi kuu ya Kenya KPL akiwa akiwa na timu yake ya Gormahia FC.
Kocha Kerr alijiunga na klabu ya Gormahia kama kocha tarehe 5, Julai 2017 akichukua nafasi ya kocha alieondoka klabuni humo Kocha Ze Maria.
Mwaka 2015 Kerr aliifundisha klabu ya Simba na kufanikiwa kuifanya kuwa katika nafasi 3 za juu kwenye msimamo wa ligi Tanzania bara.