Andy Murray aendelea kumwaga Chozi
Sura za majonzi kwa watu waliokuwa uwanjani zilitawala leo baada ya Muingereza Andy Murray kutolewa katika raundi ya kwanza ya michuano ya Australian Open 2019 na Mhispania Roberto Bautista ambaye ameshinda mchezo huo kwa seti 6-4,6-4,7-6,7-6,6-2
Majonzi haya si kwa ajili ya kutolewa kwa Muingereza huyo,31, bali yameletwa na hofu ya kutomuona mchezaji huyo akirudi uwanjani tena kushindana kutokana na majeraha ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.
Katika mkutano na waandishi wa habari ijumaa iliyopita mshindi huyo wa Grand Slam mara 3 alisema kuwa kutokana majeraha yake ya nyonga yanayomuandama alipanga kustaafu baada ya kucheza Wimbledon mwaka huu lakini akasema huenda michuano hii ya Australian Open ikawa ya mwisho kwake na kutundika daruga.
.
“ Kiukweli sina kitu chochote cha kusema. Labda tutaonana tena . Nitafanya kila litakalowezekana kujaribu kama nitataka kurudi tena . Nitatakiwa kufanyiwa upasuaji mkubwa ili kurudi tena, lakini nitafanya kadri ya uwezo wangu . Ahsanteni “ amesema Murray baada ya mchezo