“HATUWEZI KUOMBA RADHI KWA SABABU NI SEHEMU YA MCHEZO” .
Klabu ya Simba SC baada ya kumalizika kwa mchezo wake wa klabu Bingwa Afrika hatua ya makundi dhidi ya JS Saoura ya nchini Algeria, wachezaji wake Haruna Niyonzima, Rashid Juma na Shiza Kichuya walisafiri asubuhi kuelekea Pemba katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi 2019.
Simba walicheza mchezo huo wa fainali dhidi ya Azam FC ambao ndio Mabingwa watetezi wa michuano hiyo, Azam FC wameendelea kulitetea taji hilo kwa kulitwaa kwa mara ya tatu mfululizo taji hilo kwa kuifunga Simba SC kwa mabao 2-1, mabao ya Azam yakifungwa na Mudathir Yahya dakika ya 44 na Obrey Chirwa dakika ya 72 baada ya Mlipili kuisawazishia Simba dakika ya 63 kwa kichwa.
Baada ya kipigo hicho ambacho ni cha pili mfululizo kwa Simba kutoka Azam FC katika mchezo wa fainali ya Kombe la Mapinduzi, nahodha wao Haruna Niyonzima alihojiwa na Azam TV kuhusiana na mchezo huo alizungumzia kuwa timu yao ilicheza vizuri licha ya kupoteza mchezo ni sehemu ya mchezo kushinda au kushindwa.
“Kupoteza ni jambo moja kuongezeka ni jambo lingine, mimi ninaamini tumesaidia timu. Kama mwenyezi Mungu amepanga tufungwe tutafungwa hata kama tungekuwa wote, kuhusu mashabiki wa Simba waliokuwa wamejitokeza hapa na Pemba kwanza niwapongeze kwa kujitokeza siwezi kusema niwaombe radhi ni matokeo sisi wenyewe hatujapenda kupoteza mchezo wa leo ila hii imebaki ni historia kitu ambacho tunaangalia ni michezo ya mbele” alisema Haruna Niyonzima baada ya mchezo