Mchezaji wa zamani wa Afrika Kusini afariki Dunia
Mshambulizi wa zamani wa klabu ya Leeds na timu ya Taifa ya Afrika Kusini Phil Masinga amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 49.
Bado haijawekwa wazi kuhusu chanzo cha kifo chake.
Masinga aliwahi kuichezea Leeds ya Uingereza kati ya mwaka 1994 na 1996 akicheza mechi 31 na kufunga goli 5.
Katika timu ya Taifa ya Afrika Kusini amecheza mechi 58 na pia aliisaidia timu hiyo kuchukua ubingwa wa Mataifa Afrika katika ardhi ya nyumbani.