JARIBIO LA MAURIZIO SARRI WA CHELSEA KUMNASA PEREYRA LIMEGONGA MWAMBA
Kwa mujibu wa wakala wa mchezaji Roberto Pereyra wa Watford ni kuwa klabu ya Chelsea imejaribu kwa mara nyingine kutaka kumsajili mchezaji huyo na imeshindikana , wakala wa mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari vikieleza kuwa kocha wa Chelsea Maurizio Sarri ana muhitaji mteja wake.
Roberto Pereyra alijiunga na klabu ya Watford ya nchini Uingereza mwaka 2016 akitokea Juventus ya nchini Italia lakini imeripotiwa kuwa mkataba wake wa sasa na Watford unamalizika Juni 2021, tokea amejiunga na timu hiyo ameichezea sio chini ya mechi 68 hadi sasa.
Mchezaji huyo mwenye uwezo wa kucheza nafasi ya kiungo na mshambuliaji, Roberto amefunga mabao 13 na kusaidia wachezaji wenzake kufunga mabao mara nane ila kwa msimu huu amefunga mabao 6 ya Ligi katika michezo 21, kwa jitihada zake kwa sasa ndio mfungaji bora wa klabu kwa msimu huu akiwa kafunga mabao 6 akifuatiwa na Troy Deeney aliyefunga mabao 5.