Chelsea haina wa kumwogopa.
Kiungo Mbrazil Willian amerusha sifa kwa kocha wa timu yake ya Chelsea Maurizio Sarri mabadiliko aliyofanya toka ajiunge na timu hiyo majira ya joto.
Ikiwa inashika nafasi ya tatu nyuma ya Liverpool na Manchester City Chelsea haijapoteza mchezo wowote wa ligi hadi sasa siku ya Jumapili watakuwa ugenini dhidi ya Burnley iliyopo katika nafasi ya kumi na tatu.
Willian anaamini goli la Barkley dhidi ya Manchester United katika dakika za lala salama lilidhihirisha ni namna walivyojipanga kuweza pigania ubingwa msimu huu. “Tunajua ilivyo muhimu kucheza mechi kubwa na kufunga hasa dakika za lala salama”
Hatuna wa kumuogopa katika ligi msimu huu kwani tupo na timu inayoweza kupambana hadi mwisho na nina imani tutafanya hivyo.”
Kiungo huyu anaamini mabadilimo chanya yaliyotokea kwa Chelsea ambayo ilimaliza katika nafasi ya tano ikiachwa kwa points 30 na Manchester City walioibuka mabingwa amesema sifa kubwa zimwende kocha Maurizzio Sarri.
“Umekuwa mwanzo mzuri na tumecheza vizuri na sifa zote zimwendee kocha Sarri.”
“Namna anavyofanya kazi ni anahakiki tunacheza mpira mzuri na anatupa nafasi ya kuonyesha ubora wetu zaidi.”
Willian alikuwa akihusishwa na tetesi za kuondoka klabuni hapo baada na kuwa katika na uhusiano mbovu wa kazi baina yake na kocha Antonio Conte ila sasa mambo yamebadilika na amerejea katika kiwango chake bora toka kutua kwa kocha Sarri.
“Sipo hapa kuwakandia makocha waliopita sababu kila kocha na filosofia yake mwenyewe. Kila mmoja anajionea Chelsea ikiwa vizuri. Sari amekuwa mtu mzuri, mwenye akili sana na kocha mzuri anayeongea nasi kila wakati.”
“Muda mwingine amekuwa tukitaniana sana na hili sio jambo baya sababu linasaidia amsha morali katika timu.”
Maurrizio Sarri anakuwa kocha wa sita kucheza mechi nane za mwanzo za ligi bila kufungwa na wa tatu kwa Chelsea akiungana na Jose Morinho na Felipe Scolari.