Rashford kufika Level za Harry Kane
Ole Gunnar Solskjaer adai Rashford atakuwa mshambuliaji wa kiwango kikubwa kama Harry Kane.
Kuna mengi ya kuona na kusikia. Kuelekea mechi ya Manchester United dhidi ya Tottenham jumapili hii, kocha wa muda wa Manchester Ole Gunnar Solskjaer ameibuka na kudai mchezaji wake Marcus Rashford ana uwezo wa kuwa mshambuliaji wa kiwango kikubwa kama Harry Kane.
Amesema mchezaji huyo anajituma na kuweka juhudi na anazidi kuimarika kila siku.
Rashford aliyefunga magoli 7 msimu huu, yupo na safari ndefu kumfikia mshindi huyo wa kiatu cha dhahabu England mara mbili.
Kwa sasa amekuwa akitumika kama mshambuliaji wa kati tokea kuwasili kwa Ole akiwa amefunga goli 3 katika mechi 5 ikilinganishwa na goli 4 katika mechi 22 chini ya kocha aliyepita Jose Mourinho.