ADEYUN YUSSUF AMEKANUSHA TAARIFA ZA KUIGOMEA COASTAL UNION KISA MSHAHARA
Baada ya kuenea kwa taarifa mbalimbali katika mitandao ya kijamii kuhusiana na klabu ya Coastal Union ya jijini Tanga kuwa kwa sasa ipo katika hali mbaya kiuchumi kiasi cha kukimbiwa na wachezaji wake karibia wote na kusalia wachezaji 13 kikosini.
Leo tulikutana na mchezaji wa timu hiyo ya Coastal Union anayejulikana kwa jina la Adeyun Yussuf ambaye alikuwepo katika uwanja wa Amaan Unguja katika mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mapinduzi Cup 2019 kati ya Simba SC dhidi ya Malindi FC mchezo dakika 90 zikimalizika kwa 0-0.
Mchezo uliamuliwa kwa mikwaju ya penati na Simba SC kuingia hatua ya fainali ambayo watakutana na timu ya Azam FC siku ya Jumapili katika uwanja wa Gombani Pemba, hiyo ni baada ya ushindi wa penati 3-1, baada ya mchezo tuliongea na Adeyuni kwa nini ameonekana akiichezea Malindi na kuiacha Coastal.
“Mchezo ulikuwa mzuri wao walikuwa vizuri zaidi na sisi tulikuwa vizuri lakini Mungu amewajaalia wao wamekwenda fainali, nipo huku kwa sababu ya kuwa majeruhi lakini vile vile nilikuja kuoa kesho tukijaaliwa narudi katika klabu yangu (Coastal Union) hapa nafanya mazoezi tu hii mimi ndio timu yangu ya zamani, siwadai Coastal sio kweli na sijagoma ila tu leo mshahara watu washaingiziwa fresh” alisema Adeyun Yussuf Costal Union ambaye pia inachezewa na msanii wa Bongofleva Alikiba hivi karibuni ilidaiwa kuwa katika mtikisiko kidogo wa kiuchumi kupelekea wachezaji wake kugoma, kwa sasa Coastal Union ipo nafasi ya 10 ikiwa na jumla ya alama 25 ikicheza michezo 18 hadi sasa ikiwa imepoteza mechi tatu tu kati ya hizo.