MLIPILI AJINASIBU KUWA SIMBA YAO INA KIKOSI CHA KIPANA
Kwa mara ya pili mfululizo klabu ya Simba SC inafanikiwa kuingia hatua ya fainali ya michezo ya Mapinduzi Cup na itacheza tena na Azam FC kama ilivyokuwa mwaka jana katika mchezo wa fainali timu hizo zilikutana ila Azam FC akashinda taji hilo kwa mara ya pili kupitia bao la Himid Mao na kuufanya mchezo ukiwa 1-0.
Simba SC wameingia fainali kwa kuwafunga Malindi kwa mikwaju ya penati 3-1 baada ya dakika 90 za mchezo kumalizika 0-0, wakati Azam FC wanaingia fainali kwa mara ya tatu mfululizo wakiwa wamemtoa KMKM katika mchezo wa fainaili ya mapema ila baada ya mchezo wa Simba SC dhidi ya Malindi nahodha wa muda wa Simba Yussuf Mlipili aliongelea kuhusiana na mchezo huo.
Simba ambayo inacheza mchezo wa klabu Bingwa Afrika Jumamosi dhidi ya JS Saouro ya Algeria ilicheza mchezo huo dhidi ya Malindi bila uwepo wa wachezaji wao wa kikosi cha kwanza na inaripotiwa kuwa wakimaliza mchezo baadhi ya wachezaji wao watasafiri kuelekea Pemba kucheza mchezo wa fainali.
Mlipili ambaye amekuwa hana nafasi katika kikosi cha Simba cha kwanza kutokana na uwepo wa mabeki wengi waliokuwa na uwezo mkubwa dhidi yake alionekana kuwa na furaha na ushindi huo “Wana Simba siku zote huwa na wasiwasi hata kama mwalimu atakuwa anasema leo anapanga kikosi cha kwanza, yaani siku zote mashabiki wetu wanakuaga ni watu wa wasiwasi ndio lakini tumejipanga wenyewe na kupata ushindi sisi kama kawaida yetu tuna kikosi kipana, Sasa hivi nawaambia mashabiki wa Simba wafurahi tu hii ndio Simba dume” alisema Mlipili