TFF yasimamisha uchaguzi wa Yanga SC
Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la mpira Tanzania TFF Malangwe Ally Mchungahela leo Ijumaa ya Januari 11 2019 zikiwa zimesalia siku mbili kabla ya uchaguzi Mkuu wa Klabu ya Yanga, Mchungahel ametangaza kusitisha uchaguzi huo.
Kamati hiyo ya Uchaguzi ya TFF chini ya Mchungahela imefikia maamuzi ya kusitisha uchaguzi wa Yanga kwa muda usiojulikana, baada ya kupokea taarifa kuwa baadhi ya wanachama wa Yanga wapo Mahakamani kupinga mchakato huo wa uchaguzi hivyo TFF wanasubiri shauri hilo kusikilizwa.
Licha ya kuwa hazijawekwa sababu za baadhi ya wanachama wa Yanga kuzuia mchakato wa uchaguzi, ila inadaiwa kuwa ni Kundi la baadhi ya wanachama wa Yanga wanaomshinikiza kuwa mwenyekiti wao wa zamani Yussuf Manji ndio wanataka aendele kuwa katika nafasi ya uenyekiti.