Liverpool ilimfanya Aguero aumwe
Kocha wa Man City Pep Guardiola leo amesema kuwa Sergio Aguero aliumwa mara baada ya mechi dhidi ya Liverpool kumalizika.
Mchezo huo ulimalizika kwa Man City kushinda goli 2-1 na kumaliza rekodi ya kutopoteza mchezo ya Liverpool katika msimu huu ligi kuu nchini England
Kocha huyo amesema mshambuliaji huyo anaendelea vizuri na leo amefanya mazoezi yake ya kwanza.
Man City watacheza mechi yao ya ligi kuu jumatatu dhidi ya Wolves katika uwanja wao wa nyumbani Etihad