ARNAUTOVIC AZITAKA HELA ZA WACHINA
Baada ya kuletewa dau la pauni Millioni 35 klabu ya WestHam imesema mshambuliaji wao Marko Arnautovic hauzwi hata baada ya wakala na kaka wa mchezaji huyo kutaka dau hilo kupokelewa.
Msemaji wa klabu alikaririwa akisema “Marko ni ana mkataba na klabu na tunategemea atauheshimu kikamilifu na pia kwa sasa sio wa kuuza.”Inaaminika mabingwa wa ligi ya China Shanghai SIPG, wameweka mezani dau la pauni millioni 35 kwa ajili ya Arnautovic na mshahara wa zaidi ya pauni 250,000 ( Tsh Milioni 737 ) kwa wiki kwa muda wa miaka minne.
Katika mkutano wa waandishi wa habari alhamisi iliyopita kocha Manuel Pellegrini alikiri na kusema “Hizo zote ni tetesi. Marko ni mchezaji mzuri na klabu nyingi zinamuhitaji. Ila kwa sasa hatuna taarifa yeyote.”
.
“Sihitaji kuongea nini kitatokea. Marko kwa sasa ni mchezaji wa klabu hii na tupo na wachezaji wengi wa kiwango chake kama Declan Rice, Fillipe Anderson na wengine wa aina hii ambao wanaweza kuhitajika na vilabu vingine. Hivyo hilo ni jambo lingine ila sidhani kama wataondoka.”
.
“Ninahitani kumbakiza ila huwezi jua nini kitatokea.”
Arnautovic mwenye miaka 29 ameifungia klabu hiyo magoli 7 katika ligi hadi sasa msimu huu na mwishoni mwa wiki hii watakuwa uwanjani kucheza dhidi ya Arsenal.