Sterling aendelea kupambana na ubaguzi
Sterling amuandikia barua kijana shabiki wa Manchester City aliyefanyiwa ubaguzi wa rangi.
Imeelezwa kuwa mchezaji Raheem Sterling alimuandikia barua shabiki wa Manchester City aliyefanyiwa ubaguzi wa rangi.
Picha za barua hiyo zilisambaa katika usiku wa jumatano kwenye mechi ya ushindi wa goli 9 – 0 dhidi ya Burton Albion mchezo wa FA Cup.
Bibi wa kijana huyo alimtumia ujumbe Sterling na kumueleza kuwa kijana wake amekuwa akipata wakati mgumu kutokana na ubaguzi wa rangi.
.
“Simama kwa ufahari na usikubali mtu yeyote akuondolee ujasiri wako.”
.
“Usibadilike, simama kama wewe na kumbuka kuwa kuongea tu hakufanyi maisha yawe rahisi.”
.
Sterling alikuwa mhanga wa ubaguzi wa rangi katika mechi ya Manchester City dhidi ya Chelsea katika uwanja wa Stanford Bridge mwezi uliopita.
Hakusita kusimama dhidi ya hali hii na kupitia mtandao wa Instagram alivituhumu vyombo vya habari kushiriki katika kukuza tatizo hili kwa kutoa taarifa kibaguzi.
Mwezi Disemba 2017 mtu mmoja alifungwa baada ya kumfanyia Sterling ubaguzi wa rangi nje ya kiwanja cha mazoezi cha Manchester City.