Solskjaer amkaribisha Pochettino OT
Kuelekea mechi ya Tottenham na Man United katika uwanja wa Wembley jumapili hii, kocha wa mashetani wekundu Ole Gunnar Solskjaer ameongea na waandishi habari.
Katika mkutano huo kocha huyo aliulizwa kuhusu kocha wa Tottenham Maurcio Pochettino kuhusishwa kujiunga na Man United, akajibu kuwa Muargentina huyo anafanya kazi nzuri ndio maana amehusishwa na kutua hapo.
Wakati kocha huyo wa muda wa Man United akitaka kuendelea kuwashawishi mabosi ili abaki kuwa kocha wa kudumu akishinda mechi zake zote 5 za mwanzo, Pochettino bado anaendelea kuwa kipaumbele cha kuchukua nafasi hiyo Old Trafford
.
“ Amefanya kazi nzuri. Tetesi zipo kwa sababu anafanya vizuri, lakini si kazi yangu kupima (uwezo) wa mameneja wengine. Mkazo wangu upo kwangu na katika timu yangu “
.
Solskjaer pia amethibitisha kuwa kiungo Paul Pogba atakuwepo katika mechi hiyo baada ya kupona maumivu ya mguu wake aliyopata katika kambi waliyokuwa wameweka Dubai.