Andy Murray jua limezama
Mchezaji tenesi wa Uingereza Andy Murray bingwa wa grand slam mara tatu amesema alipanga kustaafu baada ya michuano ya Wimbledon mwaka huu ila michuano ya Australian Open inayoanza wiki ijayo inaweza ikawa ya mwisho kwake.
.
“Sina hakika kama ninaweza kuendelea kucheza nikiwa na maumivu haya kwa muda wa miezi mingine minne ama mitano.”
.
“Ninataka kufika Wimbledon na kumalizia safari ila sina hakika kama nitaweza.”
Gwiji huyo mwenye miaka 31 amesema yupo tayari kucheza mchezo wake wa raundi ya kwanza wa Australian Open dhidi ya Mhisapania Roberto Bautista anaeshikilia nafasi ya 22.
Mchezaji huyo aliyekuwa akishikilia nafasi ya kwanza alifanyiwa upasuaji wa mguu mwezi Januari mwaka jana na amecheza mechi 14 tu toka aliporudi mwezi Juni.
Baada ya kurudi uwanjani mwezi Juni alisimama tena mwezi Septemba ili kupata muda wa kujiimarisha na kujiweka sawa chini ya mtaalamu Bill Knowles jijini Philadelphia. Baada ya miezi minne ya kufanya kujiimarisha na kugundua bado hajaweza rudi katika ubora wake na kupoteza katika mchezo wa mazoezi dhidi ya gwiji mwenzake mchezaji namba moja duniani Novak Djokovic ni hali iliyomuumiza zaidi.
Katika mkutano wake na waandishi wa habari alisema “Sijisikii vizuri. Nimekuwa nikihangaika kwa muda mrefu.”
.
“Kwa takribani miezi 20 nimekuwa ninasumbuliwa na maumivu. Nimejaribu kufanya kila niwezalo ili mguu wangu kurudi katika hali nzuri ila bado.”
.
“Nipo katika hali nzuri kuliko ilivyokuwa miezi 6 iliyopita ila bado nipo na maumivu. Ninaweza kucheza katika kiwango ila sio katika kiwango nilichokuwa ninacheza.”
.
Mafanikio ya Andy Murray katika tenesi ni::
- Grand Slam 3
- Medali za Dhahabu za Olympic 2
- Master 1000 titles 14
- Fainali ya ATP 1
- Fainali za Grand Slam 8
- Mchezaji namba 1 Duniani kwa wiki 37