Batshuayi arudishwa Chelsea
Klabu ya Valencia imetangaza kusitisha mkataba wa mkopo wa mshambuliaji Michy Batshuayi kutoka Chelsea.
Mchezaji huyo ,25, alijiunga na Valencia mwanzoni mwa msimu huu kwa mkataba wa mkopo wa msimu mmoja, lakini sasa atarejea Chelsea au kwenda timu nyingine kwa mkopo.
Mshambuliaji huyo wa Belgium amefunga magoli matatu tu katika mechi 23 alizocheza katika klabu ya Valencia kwenye michuano yote msimu huu.