Stones amwachia nyumba mpenzi wake
Beki wa Man City na Timu ya Taifa ya England John Stones ameachana na mpenzi wake wa muda mrefu na mama mtoto wake Millie Savage.
Beki huyo,24, aliamua kuhama katika nyumba ya kifahari aliyokuwa anakaa na mpenzi wake huko Cheshire na kuhamia katika Apartment kuishi mwenyewe huko jijini Manchester.
Mama mtoto wake, Millie Savage,24, amebakia kwa nyumba hiyo ambayo Stones aliinunia miaka miwili iliyopita baada ya kupata shutuma za kufanya usaliti kwa mpenzi wake.
Millie,24, amesema tayari ameongea na mwanasheria kuhusu kuachana kwao.
Wawili hao ambao wamekuwa pamoja tangu wakiwa na miaka 12 wana mtoto mmoja wa kike mwenye umri wa miezi 18.
Familia ya mwanadada imeelezwa kuhuzunika kwa Stones kuamua kuvunja uhusiano huo na walikuwa wanaishi nae kama ndugu yao.
Stones ameripotiwa ameanza mchakato wa kuondoa tattoo ya sura ya mama mtoto wake huyo Millie ambayo imechorwa katika mkono wake.
Beki huyo alichora tattoo hiyo 2017 ili kuthibitisha uaminifu wake kwa Millie baada ya kudaiwa kumsaliti kwa kuwa na mwanadada mmoja anayeitwa Jessica Peaty.
Jessica na Stones ilielezwa walikuwa pamoja kwa miezi miwili, ukaribu wako ulianza majira ya kiangazi mwaka 2016 ambapo Stones alijiunga na Man City kutoka Everton.
Jessica alidai kuwa hakujua Stones ni mchezaji mpira na hakufahamu kama ana mpenzi wa muda mrefu.
Jessica,23, alisema kuwa Stones alimwambia ameachana na Millie lakini akaja kujua ni uongo baada ya siku moja wakiwa wote alimsikia Stones akimwambia mtu aliyekuwa anaongea nae kwa simu ‘ I love you ‘.
Kwa mujibu wa Jessica, waligombana na Stones ambaye alikuwa anasema hayupo pamoja na Millie.
Jessica akamtafuta Millie katika Instagram na kuongea na kumueleza kila kitu, na kumuuliza Millie kama bado yupo na Stones au hapana, na baada ya kujua kuwa bado wapo wote, Jessica aliomba msamaha kwa Millie na kuachana na John Stones
Millie alimsamehe Stones na baada wakatapa mtoto wao wa kwanza, na katika kuonesha uaminifu, Stones akachora tattoo ya sura ya Millie katika mkono wake wa kulia
John Stones hajawahi kusema chochote kuhusu tuhuma hizo na sasa ameamua kuvunja uhusiano na kumuachia Millie jumba hilo la kifahari pamoja na mwanae