Mourinho aondoka na mabilioni Man United
Kocha Jose Mourinho ameripotiwa kuwa alilipwa fidia ya pauni milioni 15 ( Tsh Bilioni 44) alipotimuliwa na Man United Disemba 18 mwaka jana.
Mreno huyo mkataba wake katika timu hiyo ulikuwa unamalizika msimu wa 2019/20 huku kukiwa na kipengele cha kuongeza msimu mmoja.
Malipo hayo sasa yanampa uhuru Jose kurudi katika kazi yake ya kufundisha.