Man City wafanya mauaji Etihad.
Magoli ya Kevin De Bruyne dakika ya 5 Gabriel Jesus Jesus dakika ya 30 34 57 65 Zinchenko dakika 37 Foden dakika ya 62 Walker dakika 70 na Riyad Mahrez dakika ya 83 yamefanya Man City kuondoka na ushindi wa goli 9-0 katika uwanja wao wa Etihad dhidi ya Burton Albion katika mchezo wa nusu fainali ya kombe la ligi “ Carabao Cup”
Hii imekuwa ni mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 31 City kufunga goli zaidi ya nane katika mechi moja tangu walipomfunga Huddersfield Town 10-1 katika ligi daraja la pili mwaka 1987.
Ushindi huu unafanya Man City kuwa wamefunga magoli 16 katika siku nne baada ya kuifunga Rotherham United 7-0 katika raundi ya tatu ya FA Cup jumapili iliyopita.
Mechi ya marudiano itapigwa Januari 23 Pirelli Stadium na mechi ya fainali itachezwa jumapili ya Februari 24, katika uwanja wa Wembley.
City ambao ni mabingwa watetezi wa Carabao Cup, wanataraji kukutana na Chelsea au Tottenham katika fainali.