Higuain kumfuata Sarri darajani
Klabu ya Chelsea imeripotiwa kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji Gonzalo Higuain, kwa mujibu wa mtandao wa Marca wa nchini Hispania.
Timu hiyo imekuwa ikihusishwa na kumsajili mchezaji huyo katika wiki za hivi karibuni ambapo kocha wao Maurizio Sarri akiwa na lengo la kusajili mshambuliaji mpya.
Ripoti zinasema kuwa, Higuan alisema ndio alipoambiwa kuhusu kutua Stamford Bridge.
Muargentina huyo sasa anacheza kwa mkopa AC Milan akitokea Juventus, na imeelezwa timu hizo zote zipo tayari kwa dili hilo.
Gonzalo Higuain alikuwa mwiba katika msimu mmoja (2015/16) ambao alikuwa chini ya Sarri katika klabu ya Napoli, akifunga jumla ya goli 38