Griezmann amkimbiza Messi LaLiga
Nyota wa klabu ya Atletico Madrid Antoine Griezmann ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwezi Disemba katika ligi kuu nchini Hispania LaLiga
Griezmann katika mechi nne alizocheza katika La Liga mwezi Disemba, amefunga magoli manne na kutoa Assist moja.
Mfaransa huyo ndiye mchezaji aliyeshinda tuzo hiyo zaidi kuliko mchezaji mwingine yoyote, ameshinda mara 6, huku Lionel Messi akiwa wapili akichukua mara 4, Cristiano Ronaldo na Luis Suarez wakiwa nafasi ya tatu ambapo kila mmoja ameshinda mara tatu.