Bailly amfuata Lukaku Roc Nation
Beki wa Man United Eric Bailly amejiunga na kampuni ya usimamizi ya Roc Nation Sports Agency inayomilikiwa na msanii wa Marekani Jay Z.
Bailly,24,anaungana na mchezaji mwenzake wa Man United Romelu Lukaku na Jerome Boateng wa Bayern Munich katika kampuni hiyo.
Roc Nation Sports ni tawi la kampuni ya Roc Nation, kampuni ya burudani iliyoanzishwa na Jay-Z
Tawi hilo la michezo lilianzishwa mwaka 2013 na likiwa na lengo la kusaidia wanamichezo ndani na nje ya uwanja kama vile masuala ya kibiashara, vyombo vya habari na mipango ya kujenga jina ( Brand)